22 November 2010

NANI KUWA MEYA JIJI LA ARUSHA?

 Mussa Juma, Arusha.

MADIWANI watano wa chama cha mapinduzi katika jiji la Arusha, wamejitokeza kuwania nafasi za Meya wa jiji na Unaibu meya wa jiji la Arusha.

Katibu wa CCM wilaya ya Arusha, Salum Mpamba akizungumza na mwananchi jana jioni aliwataja waliochukuwa fomu na kurejesha kwa upande wa Meya ni Paul lota Laizer diwani wa kata ya  Baraa, Gaudence Lymo diwani wa Olerien na   Paul Mathsen diwani wa kata ya Mushono.

Alisema kwa upande wa Naibu Meya waliochukuwa fomu ni Julias Sekeyani wa kata ya Terati na Alfonce Mawazo wa kata ya Sombetini.

"hadi sasa mwisho wa kuchukuwa fomu ni hao madiwani watano wamejitokeza na tunasubiri vikao vianze kuwajadili na baadaye kupitisha jina moja kwa kila nafasi"alisema Mpamba.

Hata hivyo,.alisema wakati jana ilikuwa mwisho ndani ya CCM kuchukuwa fomu, bado idadi ya viti maalum vya udiwani ambavyo kila chama inapaswa kuvipata haijajulikana.

" ni kweli majina ya viti maalum bado ila majina ya wagombea hawa yanahitajika mapema ili kujadiliwa na vikao"alisema Mpamba.

Wagombea hao, wa CCM wanatarajia kuchuana kwa nafasi ya Umeya, na wagombea wa chadema ambapo tayari jina la Estomii Malla diwani wa kata ya Kimandolu  limepitishwa huku nafasi ya unaibu Meya majina matatu yanatajwa ambao ni John Bayo wa kata ya Elerai chadema,diwani wa Michael Kivuyo wa TLP na Charles Mpanda wa cxhadema kata ya kaloleni.

Katika jiji la Arusha CCM ina madiwani 10, chadema 9 pamoja na Mbunge nma Tlp mmoja lakini bado idadi ya viti maalum haijatolewa ambayo inaweza kuongeza idadi ya madiwani wa chadema na hivyo kuongeza halmashauri ya jiji la Arusha

MWISHO