17 December 2010

 Nenda hifadhi ya Mahale ushuhudie haya;
Nenda mahale ukaone sokwe hawa. picha zaidi za ziara ya wanahabari katika ziara ya hifadhi 14 za Taifa  zaja  tembelea blog hii
unawajua sokwe mtu, ndio huyu nyuma ya mussa juma, ndani ya hifadhi ya Taifa ya Mahale mkoani kigoma tembelea ujioneaa
pichani ni baadhi ya wanahabari wakiwa ndani ya boti katika ziwa Tanganyika wakiwa katika kazi ya kuhamasisha utalii wa ndani.
the media which a visit every day is mwananchi ,outside the count

05 December 2010

VITA dhidi ya UKIMWI na wanahabari

 pichani ni waliokaa kwenye viti ni mbunge jimbo la Arusha,chadema Godbless Lema akiwa na mbunge chadema viti maalum mkoa Arusha ,Joyce Mukya,   meneja wa PSI mkoa wa Arusha na Manyara, Chris Mbajo, mratibu wa TACAIDS mkoa wa Arusha na  Mkurugenzi wa  kampuni ya Ms Unique Mussa juma   na mratibu wa semina Upendo Simwita ,picha hii ilipigwa  mara baada ya kufunguliwa  na Lema semina ya waandishi wa habari mkoa wa Arusha kuhusiana na ugonjwa wa UKIMWI semina hiyo iliandaliwa na kampuni ya ms unique promotion  ya Arusha

03 December 2010

Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania, Dietlof Mare akimshukuru na kumpongeza Elifuraha Paul Mtowe mfanyakazi mwanzilishi wa Vodacom katika Kanda ya Kaskazini ya Tanzania ambaye amehusika kwa kiasi kikubwa kufundisha huduma za kampuni hiyo kwa umma, kukuza biashara, kupanua mawasiliano na kuwajengea wakazi wa Kanda ya Kaskazini Imani kwa Vodacom, Kuipenda, Kuiheshimu na Kuitumia kampuni hiyo katika huduma za mawasiliano hali inayoifanya Vodacom kubakia mtandao mkubwa na unaoheshimika kwa Kanda hiyo na Tanzania kwa ujumla.
 madereva wengine ni hatari, hapa kaparamia daraja akikwepa kogonga basi la abiria maarufu kama kifodi jijini  Arusha jana.

wabunge wa chadema na wanahabari mara baada ya semina ya HIV

 mbunge wa jimbo la Arusha, Godbless Lema akiwa na mbunge wa viti maalum mkoa wa Arusha, chadema JoyceMukya wakizungumza na baadhi ya waandishi wa habari mkoani Arusha mara baada ya kufungua semina ya masuala ya UKIMWI kwa wanahabari ambayo iliandaliwa na kampuni ya MS unique kwa kushirikiana na TASWA Arusha .

Wanahabari na vita dhidi ya UKIMWI.

WAANDISHI wa habari nchini, wameombwa kujiepusha na vitendo hatarishi ambavyo vinachangia maambukizi dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi.

Mbunge wa Jimbo la Arusha,Godbless Lema, alitoa wito juzi  wakati akifungua semina ya siku moja ya waandishi wa habari mkoani Arusha juu ya masuala ya UKIMWI ambayo ilifanyika Ricks Morden klabu .


Lema alisema waandishi wa habari kama wanajamii wengine, wanakabiliwa na tishio kubwa la maambukizi ya UKIMWI kutokana na mazingira ya kazi zao.

“nawapongeza  waratibu wa semina hii na mimi kama mbunge nawahakikishia tutaendelea kushirikiana wakati wote kama masuala haya ya kijamii”alisema Lema.

Akitoa mada katika semina hiyo,Dk Saimon Megiroo  toka hospitali ya Selian mkoani hapa, alisema wanahabari ni wadau muhimu sana katika vita dhidi ya Ukimwi kama wakitumia kalamu zao kuelimisha vyema jamii.

“Selian tuna kitengo cha masuala ya Ukimwi na moja ya wadau wetu katika masuala ya uelimishaji ni wanahabari”alisema Dk Migiroo.

Naye Meneja mahusiano ya shirika la mtandao wa wafugaji PINGOS Forum Stivin Shikuku akitoa mada katika semina hiyo, alisema  jamii za wafugaji  bado zinaathirika sana na ukimwi kutokana na kutokuwa na elimu ya kutosha.

Akitoa mada juu ya tafiti za vita dhidi ya UKIMWI katika jamii hizo, alisema bado huduma muhimu  za  afya kama upimaji na upatikanaji wa dawa za kurufusha maisha katika jamii hizo  hazipatikani.

Awali Meneja wa shirika la PSI mkoa wa Arusha na Manyara, Chris Mbajo akitoa mada yake juu ya kujikinga na maambukizi mapya ya UKIMWI aliwataka wanahabari kuhakikisha wanajiepusha na vitendo vitakavyo wafanya wapate maambukizi.

Semina hiyo ya wanahabari iliyodhaminiwa na mamlaka ya hifadhi Ngorongoro, shirika la wafugaji la Pingos Forum, iliandaliwa na chama cha waandishi wa michezo mkoa Arusha(TASWA) kwa ushirikiano na kampuni ya Ms Unique na chama cha wanaoishi na virusi cha Tumaini Positive(TUPO).
MWISHO.

baraza la mawaziri la maridhiano ndani ya CCM lina jipya

Tutegemee nini  Baraza la mawaziri la maridhiano ndani ya CCM.

                                    Mussa Juma.

MAWAZIRI  50 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , wameapishwa ,huku kukiwa na sura mpya 24 na sura zilizozoeleka ndani ya baraza hilo 26.

Uteuzi huu ambao umefanywa na Rais Jakaya Kiwete, umepokelewa kwa hisia tofauti na wadau mbali mbali wa masuala ya siasa, wapo walipongeza, wapo walioomba mawaziri kupewa muda na wapo ambao wanaamini baraza hili ni vigumu kutekeleza Ilani ya uchaguzi wa CCM.

Wanaotilia shaka baraza hili, wanahoja mbali mbali kwanza wanaona bado ni kubwa,pili sura nyingi ni zile zile na pia ahadi za CCM zilikuwa nyingi sana katika uchaguzi uliopita hivyo kutekeleza zote ni ndoto ya mchana.

Lakini kikubwa zaidi katika baraza hili ni kuonekana  ni baraza la maridhiano ndani ya CCM kutokana na mawaziri wengi ambao hawakuwa wanamtando kupewa nafasi  katika wizara zenye majukumu makubwa.

Uteuzi wa baadhi ya mawaziri  na kupewa wizara kubwa nje ya mtandao  pia umepokelewa kwa hisia tofauti na wadau wa masuala ya siasa.

 Wapo wadau   ambao sasa wanaamini Rais Kikwete kaamua kuweka kanda wapiganaji makubwa wa mtandao uliosaidia ushindi wake mwaka 2005  na wapo wanaoamini sasa ameamua   kuzima manunguniko ya baadhi ya wanasiasa wakongwe na  Wananchi kuhusu uteuzi ambao amekuwa akiufanya.

Baadhi ya Mawaziri ambao wanaaminika hawakuwa katika mtandao na sasa wapo katika wizara nyeti ni kama John Magufuli,ambaye ni Waziri wa Ujenzi, George Mkuchika waziri wa TAMISEMI,Dk Harryson Mwakyembe Naibu Waziri ujenzi,Shamsi Vuai Nahodha waziri mambo ya ndani,Lazaro Nyarandu Naibu waziri wa Viwanda na biashara na wengine kadhaa.

Ingawa kuna mawaziri wengine hawakuwa katika mtandao hata katika baraza lililopita na sasa wamerejeshwa katika uwaziri na kupewa wizara kubwa, kama Profesa Mark Mwandosya, Waziri wa Maji, kuteuliwa kwao kuna ishara kubwa ya muafaka ndani ya CCM.

Ni kweli usiofichika kuwa kuna baadhi ya mawaziri katika baraza lililopita waliokuwa wanamtandao na wengine hawakuwa wanamtandao, walionekana kupwaya sana katika nafasi zao na hata kufikia hatua ya kukosa mvuto katika jamii.

Lakini sasa baraza hili, kuna mawaziri  na manaibu wao kadhaa ambazo hawakuathiriwa  sana na mtandao na siasa za makundi ndani ya CCM na hivyo kutoa tumaini jipya  la kuona baraza la mawaziri linafanyakazi kwa pamoja na kwa ufanisi mkubwa.

Ninanavyo mimi baraza hili la maridhiano ndani ya CCM, linaweza kuwa na mafanikio makubwa kama wote walioteuliwa wakiamua kufanya kazi kwa maslahi ya Umma na kujitenga na siasa za makundi ya awali.

Na pia baraza hili, linaweza kumsononesha Rais Kikwete kama aliyowateua wakiendeleza makundi yao na hivyo kuhujumiana wao kwa wao.

Makundi  ndani ya CCM yamekipa chama hicho, msukosuko mkubwa kuanzia ndani ya chama hadi katika bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na hata kusababisha bunge la tisa chini ya aliyekuwa Spika, Samweli Sitta kufikia maamuzi mazito ya kihistoria.


Kwa upande mmoja migongano wa wakubwa hawa ndani ya CCM imekuwa na manufaa   kwa wananchi na upande mwingine pia umekuwa na athari kwa wananchi hasa pale miradi muhimu ya kijamii inapotelekezwa kwa kuzingatia tu aliyeasisi hayupo katika kundi Fulani.

Katika mazingira ya sasa kwa baraza hili, wengi hawatarajii tena kuibuliwa mambo mazito ambayo yanaweza kuitikisa serikali ya Rais Kikwete, hii inatokana na   muundo wa baraza hili.

Baraza  hili linaweza kurejesha nguvu ya CCM katika uchaguzi mkuu ujao mwaka 2015 au kukimaliza chama hicho, hasa pale mawaziri hawa na wabunge wote wa CCM watakapoamua kusimama kidete na kutetea maslahi ya chama chao badala ya maslahi ya umma.

Uteuzi huu pia unaweza ukawa mwisho wa umaarufu wa waliokuwa wabunge wapiganaji dhidi ya ufisadi kama, Waziri wa Afrika ya Mashariki, Samweli Sitta na Naibu waziri wa Ujenzi Dk Harryson Mwakyembe. kama watakuwa kimya kuzungumza hata   yale mambo   waliyoyasimamia na kuyapinga katika bunge lililopita.

Hata  hivyo, bado ni imani ya wengi kuwa, mawaziri hawa 50 licha ya kuwa mawaziri watatetea maslahi ya umma kwa nguvu zao zote na kujitenga na kutumia nafasi zao kwa manufaa yao .

 Mawaziri hawa, wananafasi kubwa  ya kubadilisha historia ya taifa hili, pale watakaporuhusu mijada muhimu bungeni na kutoa majibu yenye tija katika masuala ya msingi yanayolalamikiwa  na watanzania.

Miongoni mwa mambo hayo ni kuhakikisha watanzania wananufaika na rasilimali za nchi yao, kuhakikisha Tanzania inakuwa na katiba mpya na pia kuhakikisha vita dhidi ya vitendo vya Rushwa na ufisadi, madawa ya kulevya, matumizi mabaya ya madaraka vinapiganwa kwa dhati na sio kwa maneno matupu.

Lakini kama baraza hili,litarejea kule tulipotoka katika siasa za makundi,siasa za kutetea maslahi binafsi, siasa za kuchafuana ni wazi  matarajio ya walio wengi yatakuwa yametoweka na baraza hili halitakuwa  tena baraza la maridhiano ndani ya CCM bali litaongeza mpasuko.

mussa juma ni mwandishi wa mwananchi mkoa wa Arusha, anapatikana  0754296503 email mussa_juma@yahoo.com,mussanews.blogspot.com

MWISHO.