01 February 2014

Waziri Mkuu Mizengo Pinda alipotua Kiteto kusuluhisha mgogoro wa ardhi na kutaka wavamizi kuondoka eneo la hifadhi la Emburey Murtangos.anayemsalimia ni Mkuu wa wilaya ya Kiteto, Martha Umbulla
watoto wa jamii ya kimasai kijiji cha Ngiligish wilayani Kiteto wakiwa wamepumzika nje ya nyumba yao iliyochomwa moto kutokana na mgogoro wa ardhi baina ya wafugaji na wakulima wilayani Kiteto mkoa wa Manyara
mkuu wa mkoa wa Manyara, Elaston Mbwilo, akifafanua mgogoro baina ya wakulima na wafugaji Kiteto na kueleza lazima serikali itawaondoa wavamizi wote
kamanda wa polisi mkoa wa Manyara, Akili Mpwapwa akielezea opereshemi za kusaka waliohusika na mauwaji ya wakulima 9 na mfugaji mmoja wilayani Kiteto, watu 12 tayari wamefikishwa mahakamani kwa mauwaji hayo, yaliyotokea januari 12 mwaka 2014
binti wa miaka 12 aliyeolewa akizungumza na waandishi pamoja na mkuu wa LHRC mkoa wa Arusha,Shilinde Ngalula
mkurugenzi halmashauri kiteto, akifafanua jambo
dc kiteto; martha umbula akifafanua juu ya mgogoro wa ardhi kiteto
kiteto lazima kuingia ndani kujua uhalisia wa mambo
kazi mwenyekiti wa halmashauri ya Kiteto akifafanua mambo