25 November 2010

kampeni za udini katika siasa za tz

Tutegemee vyama vya kianglikana na kianswar sunna uchaguzi ujao  
                      Mussa Juma

IMEKUWA ni kawaida kila wakati wa uchaguzi kuibuliwa hisia za kidini miongoni mwa vyama vya siasa na wagombea.
 
Hisia hizo za kidini,  zimekuwa zikitumiwa kama mtaji wa vyama pale  ambapo chama kimoja kitakapotuhumiwa ni cha kidini.
 
Kwa bahati mbaya sana propaganda za siasa za kidini zimekuwa zikitumiwa kudhoofisha vyama vya upinzani hasa pale  chama  kimoja  kinapoonekana kuwa na nguvu.
 
Dhana ya udini ilianza kupamba moto katika chaguzi za mwaka 2005 pale  ilipotumika  kukidhoofisha  chama cha  wananchi CUF  baada ya kukituhumu kuwa ni cha kiislam.
 
Katika uchaguzi wa mwaka huu, tuhuma zile zile zilizopunguza nguvu ya CUF, zimehamia chadema na sasa baadhi ya viongozi wa kisiasa na kidini wamesikika wakikihusisha chama hicho na kikristo.
 
Bila aibu wala hofu ya kutumia siasa za dini kuwagawa watanzania, baadhi viongozi katika uchaguzi wa mwaka huu, wameweza kutumia dhana hiyo ya udini kwa mafanikio japo si yale yaliyokusudiwa.
 
Katika siasa hizi za kidini, kwa bahati mbaya zaidi baadhi ya viongozi wa dini  wamekuwa wakijikuta wakiingizwa kuzishabikia bila hata wao kufanya tafiti na kujua athari za matamko yao .
 
Ingawa viongozi hawa wa dini, wanamapenzi na vyama vya siasa lakini baadhi wameshindwa kufisha hisia zao na kuchotwa na wanasiasa na hivyo kutumika kama vipaza sauti vya vyama fulani.
 
Mara nyingi imetokea  baadhi ya viongozi wa dini, kujikuta wakiwa washabiki wa chama tawala na kutoa matamko tata yasiyo ya kidemokrasia  na hapo hupongezwa na hakuna ambaye hutamka kuwakosea viongozi hao.
 
Katika uchaguzi wa mwaka 2005, kuna baadhi ya viongozi wa dini walipaza sauti zao na kutamka kuwa,aliyekuwa mgombea wa CCM wa Urais wa chama tawala ni chaguo la mungu.
 
Waliopaza sauti hizo walipongezwa kila kona na hakuna ambaye aliwaonya kuwa wanaeneza siasa za kidini.
Wengine walitumia madhabahu yao , kukituhumu chama cha CUF wakati huo ni cha kidini na kuwasihi watanzania kuwa makini na  chama hicho.
 
Hata hivyo, kila baya lina uzuri wake, kuhusisha chama na dini Fulani kumesaidia vyama hivyo kupata wanachama ambao ni watiifu wa dini zinahohusishwa na chama.
 
Hili lipo wazi tangu ipazwe sauti kuwa  CUF ni chama cha waislam kimesaidia maeneo yenye waislam wengi kukiunga mkono chama hicho na hili lipo wazi.
 
Na katika uchaguzi wa mwaka huu, pale chadema walipohusisha na ni ya kikristo kuna maeneo mengi, kumesaidia wakristo kukipigia kura chama hicho na hata kutwaa majimbo muhimu kama Arusha mjini.

Sidhani kama walivumisha sauti hizi za udini, wamejifunza katika hilo japo kuwa sasa chama cha udini cha mwaka 2005 kimeunda serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar .
 
Hata hivyo, wakati vyama vya CUF na Chadema vikihusisha na dini chama tawala kimekuwa  kisafi hakina dini ni cha kipagani na ni cha wote, lakini je matamko haya yana manufaa.
 
Kama tukiachia hili tusishangae chaguzi zijazo kuna vyama vitaingizwa katika madhehebu fulani kwani dini mbili tayari zimetumika,  sauti zitapazwa chama hiki ni cha   Kiangilikana na hiki ni cha Answar Sunna  na hapo tutakuwa tumefika pabaya zaidi.
 
Tukifikishwa katika siasa za madhehebu  watatueleza kuwa  dhehebu hili linakubali matendo haya na hili ni lazima ufanye matendo haya na hapo tutakuwa tumekwisha watanzania.
 
 Nionavyo mimi kwa ujumla wake kuhusisha chama na dini fulani ni jambo la hatari sana na athari zake ni kubwa kama  na  vurugu za kidini historia zinaonesha zimekuwa hazidhibitiki tutazame Israel na Palestina na hata tutazame yanayofukuta Sudan na nchi nyingine za Ulaya.
 
 
Binafsi sihusishi chama chochote na dini yoyote kwani kihistoria katika mapambano yoyote lazima kupata kwanza wafuasi wa kundi fulani ambao watakuunga mkono zaidi na kuungwa mkono huko hakuna maana ndio msingi wa chama au wapiganaji wote.
 
Wakati wa kudai uhuru historia inaeleza wazi kuwa Waislam wa jijini Dar es Salaam na Pwani walimuunga sana mkono sana hayati Baba wa Taifa mwalimu Julias Nyerere  katika harakati za kudai uhuru .
 
Baadhi ya Waislam wa Dar  es salam walifikia hatua ya kumuingiza msikini hayati Nyerere ,kumchagia sadaka na  kufunga kwa ajili yake na hata kumtaka  yeye kufunga na hata walimfanyia swala maalum.
 
Lakini hakuna ambaye alihusisha chama cha  TANU kuwa ni chama cha kiislam, japo kuwa wafuasi wake wengi wakati huo hata wale waliokuwa wakimuwezesha Mwalim Nyerere walikuwa waislam.
 
Hivyo hata sasa binafsi siwezi kusema chama chochote ni cha kidini hivi vyama ni vya watu wenye dini zao, imani tofauti lakini wanamawazo yanayofanana na mitazamo inayofanana katika kufikia malengo ya kushika dola.

Kwa msingi huu hiyo nina matatizo makubwa na baadhi ya viongozi wa kisiasa na kidini ambao katika karne hii ya 21 wanataka kuturejesha katika mawazo na mitizano mgando kwa kuhusisha dini na vyama vya siasa vilivyopo sasa.
 
Naamini viongozi hawa wanaotulazimisha tuanze kumwamini mtu kwa kupitia dini yake wamefilisika kimawazo na wamekosa jipya la kuwaridhisha watanzania waliowengi ambao maisha yao ni magumu.
 
Hivyo ushauri wangu ni kwa viongozi wetu wa kisiasa na kidini waache kuzitumia dini kwa maslahi yao , nawasihi sana waache mifumo ya kidemorasia ifanye kazi na hivyo tupate viongozi wiliobora na sio bora viongozi.
 
Mussa juma ni mwandishi   Arusha anapatikana simu 0715 296503, email mussa_juma@yahoo.com,mussanews.blogspoti.com.
 mwisho

22 November 2010

NANI KUWA MEYA JIJI LA ARUSHA?

 Mussa Juma, Arusha.

MADIWANI watano wa chama cha mapinduzi katika jiji la Arusha, wamejitokeza kuwania nafasi za Meya wa jiji na Unaibu meya wa jiji la Arusha.

Katibu wa CCM wilaya ya Arusha, Salum Mpamba akizungumza na mwananchi jana jioni aliwataja waliochukuwa fomu na kurejesha kwa upande wa Meya ni Paul lota Laizer diwani wa kata ya  Baraa, Gaudence Lymo diwani wa Olerien na   Paul Mathsen diwani wa kata ya Mushono.

Alisema kwa upande wa Naibu Meya waliochukuwa fomu ni Julias Sekeyani wa kata ya Terati na Alfonce Mawazo wa kata ya Sombetini.

"hadi sasa mwisho wa kuchukuwa fomu ni hao madiwani watano wamejitokeza na tunasubiri vikao vianze kuwajadili na baadaye kupitisha jina moja kwa kila nafasi"alisema Mpamba.

Hata hivyo,.alisema wakati jana ilikuwa mwisho ndani ya CCM kuchukuwa fomu, bado idadi ya viti maalum vya udiwani ambavyo kila chama inapaswa kuvipata haijajulikana.

" ni kweli majina ya viti maalum bado ila majina ya wagombea hawa yanahitajika mapema ili kujadiliwa na vikao"alisema Mpamba.

Wagombea hao, wa CCM wanatarajia kuchuana kwa nafasi ya Umeya, na wagombea wa chadema ambapo tayari jina la Estomii Malla diwani wa kata ya Kimandolu  limepitishwa huku nafasi ya unaibu Meya majina matatu yanatajwa ambao ni John Bayo wa kata ya Elerai chadema,diwani wa Michael Kivuyo wa TLP na Charles Mpanda wa cxhadema kata ya kaloleni.

Katika jiji la Arusha CCM ina madiwani 10, chadema 9 pamoja na Mbunge nma Tlp mmoja lakini bado idadi ya viti maalum haijatolewa ambayo inaweza kuongeza idadi ya madiwani wa chadema na hivyo kuongeza halmashauri ya jiji la Arusha

MWISHO

19 November 2010

biashara ya matunda

soko la matunda yanayozalishwa nchini bado ni tatizo je tatizo ni  nini

Dk Slaa na kura zake

Aliyekuwa mgombea urais wa chadema, Dk Wilbroad Slaa akipiga kura--- Je na kura yake hii ilichakachukuliwa Karatu.

vijana wa CCM hawataki viongozi wa ccm wilaya arusha

 pichani ni baadhi ya vijana wa CCM wilaya ya arusha wakiandamana kutowataka viongozi wa CCM wilaya ya Arusha kwa tuhuma za kumuhujumu aliyekuwa mgombea ubunge wa CCM jimbo la Arusha Dk Batilda Burian ambaye alishindwa na mgombea wa chadema  Godbless Lema.

mfanyabiashara wa ndizi mto wa mbu

Bibi huyu ni mfanyabiashara wa ndizi katika mji wa mto wa mbu wilayani Monduli- jimbo la aliyekuwa waziri mkuu Edward Lowassa

watafiti wa simba Serengeti

watafiti wa simba Serengeti wanajua simba huyu alipo?

barabara ya kutoka serengeti kwenda msoma mjini

huu ndio usafiri wetu barabara hii kuna askari trafik

siasa za karatu ndio hizi

 JK alipofika karatu  kwenye kampeni, alipokelewa na mamia ya vijana wakiwa wamevaa fulana za CCM, wengi hawakuelewa na kuna magazeti yaliandika JK avunja ngome ya chadema karatu, ila hapa ni vijana wale wale wakiwa katika maandamano ya kumpongeza mbunge mteule wa chadema karatu, mchungaji Israel Yohana Natse.

wanyama waongezeka serengeti

 tembelea hifadhi na uone haya hapa ni ndani ya hifadhi ya serengeti

17 November 2010

breakingnews

Meghji, Nahodha, wateuliwa kuwa wabunge
Shamsi Vuai Nahodha
Zakia Hamdani Meghji
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116539

E-mail: press@ikulu.go.tz

Website: www.mawasilianoikulu.go.tz

Fax: 255-22-2113425

PRESIDENT’S OFFICE,

THE STATE HOUSE,

P.O. BOX 9120,

DAR ES SALAAM.

Tanzania.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, amefanya uteuzi wa Wabunge watatu (3) kwa mujibu wa Ibara ya 66 (1) (e) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, kama ilivyorekebishwa na kupewa mamlaka ya kuteua Wabunge 10.

Wabunge walioteuliwa ni Ndugu Shamsi Vuai Nahodha, Prof. Makame Mnyaa Mbarawa na Ndugu Zakia Hamdan Meghji.

Rais atateua wengine waliosalia siku zijazo.

Rais Kikwete ameshawasilisha majina ya wateule hao kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Anne Semamba Makinda (Mb) kwa ajili ya hatua zipasazo.
MWISHO

Imetolewa na Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu.
Dodoma

17 Novemba

15 November 2010

arusha

My Name Mussa Juma(34) Years Old, Journalist Mwananchi news paper Arusha Tanzania .PLZ view news from my blog every day